Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Obama amesema awamu ya kwanza
ilikuwa ni kwa ajili ya kuandaa serikali ya pamoja na yenye kuaminika
nchini Iraq. Kitu ambacho amesema kimefanyika, na kuongeza kwamba
muungano huo wa kijeshi unaopambana dhidi ya kundi hilo la wapiganaji
unajiandaa kwa mashambulizi.
Tulichojua ni kwamba awamu ya kwanza
iulikuwa ni kupata serikali ya umoja wa Kitaifa na ya uhakika Iraq. Na
tumefanya hicho. ''..Na sasa tulichofanya ni zaidi ya kulimaliza nguvu
kundi hilo la ISIL.Kwa sasa tupo katika nafasi ya kuanza tena mashambulio kama ya awali. Mashambulizi ya anga yaliyofanywa yalifanikiwa katika kushusha uwezo wa kundi hilo la ISIL na kupunguza nguvu hatua waliyopiga.
Sasa tunachohitaji ni jeshi la ardhini, Jeshi la ardhini la Iraq, litakaloweza kuwarudisha nyuma..'' Nchini Iraq kwenyewe maafisa wanasema jeshi limekuwa likipiga hatua katika jihada za kuwaondoa wapiganaji hao wa kiislamu katika mji wa Baiji.
CHANZO.BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni