Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 13 Novemba 2014

UKIWEKA VOCHA UWA UNAKATWA NA UJAKOPA? GHAFLA VOCHA YAKO INAKWISHA?SERIKALI IMELIONGELEA HILO

DSC05550
Watumiaji wengi wa huduma ya simu za mkononi wamekuwa wakilalamikia wizi wa pesa unaofanywa na baadhi ya makampuni hayo, leo katika kikao cha Bunge Dodoma Serikali  imesema inatambua kuhusu wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi na kutoa tamko namna ambavyo imejipanga kukabiliana na wizi wa aina hiyo.
Akitoa tamko hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema Serikali itaanzisha kituo maalum cha kushughulikia malalamiko hayo CCC, kitakachokuwa kinasimamiwa na TCRA.
Akiuliza swali kuhusiana na jinsi Serikali ilivyojipanga  kukabiliana na wizi huo Mbunge wa Konde Khatib Said Haji amesema; “… Wizi huu unaofanywa na makampuni ya simu si wizi mkubwa kama ule wa ESCROW..  ni wizi mdogo mdogo unaowaibia Watanzania elfu tano elfu tatu lakini kwa ujumla wake, Mpemba aliyeko Konde akiibiwa elfu tatu, Mnyamwezi wa Tabora elfu mbili, Ukizijumlisha ni mamilioni ya shilingi wanaibiwa Watanzania… Leo watu hao elfu tatu elfu mbili unawaambia wapeleke malalamiko yao, gharama hiyo umeikadiriaje hata mtu huyo akadai malalamiko ya elfu tatu..”
“.. Hivi serikali yenu makini imekuwa wapi muda wote mpaka kukiri kama Watanzania wamekuwa wakiibiwa na bila wenyewe kujijua?, na bado hamna hatua mlizozichukua, ni nani aliyeko nyuma ya pazia hili la kuibia Watanzania na ninyi mkaridhia ama ni yale yaliyosemwa kama CCM ina fund katika wizi huu..?”- Khatib Said Haji.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba amesema; “…Napenda nikiri tatizo la wizi au dhuluma kwa wateja lipo na ndio lililopelekea tukaweka hizi kanuni ambazo zinaweka adhabu na hatua za kuchukua katika kuchukua katika kudhibiti wizi huo.. Licha ya utaratibu wa kawaida wa kulalamika katika makampuni  ya simu, kwa sababu moja ya matakwa ya sheria ni kwamba kampuni za simu zinapaswa kuweka utaratibu wa kuhudumia watekja wake, lakini tumebaini kwamba utaratibu huo una matatizo, unaweza ukapiga  simu muda mrefu isipokelewe, unaweza kuambiwa usubiri na wakati unasubiri kulalamika pia unakatwa..
Kwa hiyo Serikali inafahamu hilo, pamoja na hatua tulizozichukua ni kuweka ule mtambo wa kufuatilia mawasiliano ambao moja ya kazi yake sio kufuatilia tu mapato lakini ubora wa mawasiliano.. Kwa kutambua kuwa makampuni ya simu haya wakati mwingine yanachelewa wakati mwigine yanapuuza wateja, kituo hiki ambacho tunakianzisha namba zake zitasambazwa kila mtu atakuwa nayo, kwa hiyo huna haja kusafiri kufuatilia shilingi elfu mbili elfu tatu elfu tano. Kutakuwa na namba ambayo ni bure kupiga..”- January Makamba.
“ Kila utakapopiga kulalamika utapewa namba maalum ya lalamiko lako, na lisiposhughulikiwa hata kitengo cha kampuni ya simu kutoshughulikia lalamiko lako na yenyewe itakuwa sababu ya makampuni hayo kuadhibiwa..”- January Makamba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni