KWA WALE WASIOJUA MAANA YA NDOA WASOME HAPA
NDOA NINI ???
Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda
wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).
i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.
ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.
iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.
Mpango na utaratibu wa MUNGU kwa wanandoa umewekwa wazi katika kitabu cha Mwanzo.
“Bwana MUNGU akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufafana
naye”. Mwanzo 2:18.
Hapa tunaona kuna suala la mamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
“Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao
watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.
Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa
kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.
i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe
ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana
iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

TENDO
LA NDOA
Ukizingatia kanuni za MUNGU kibiblia kuhusu tendo la ndoa kwa wanandoa;-i) Ni tukio dogo lenye umuhimu mkubwa.
ii) Kusudi kubwa la tendo la ndoa ni uzazi.
iii) Ni kinga dhidi ya majaribu.
iv) Ni burudani/starehe.
v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.
v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.
NDOA -TAASISI
TAKATIFU
Ndoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake
katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa
yenye mafanikio.
i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.
ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.
iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.

NDOA NI KUTOA
1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
Hapa tunajifunza1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.
i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke
(mst.31)
ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)
iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO
anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)
2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo yawengine.
Hapa tunajifunza
i) Kutokuwa wabinafsi
i) Unyenyekevu
iii) Roho ya kutoa na kujitoa.
Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama KRISTO anavyolipenda Kanisa lake? Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesa kwa kanisa lake.
MC.RAY
WHATSAPP 0659/375263
INSTAGRAM MC.RAYMONDMUSHI
FACE BOOK Raymond Mushi
PAGE Rayshughuli
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni