Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 12 Novemba 2014

SIFA KUMI (10) ZA KUJUA MPENZI ANAEKUPENDA.



 Binti aliyetendwa na mpenzi wake aliyempenda sana.
 Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu .

1. Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.Kwa kuwa ana mapenzi ya dhati na anajua mahitaji yako , hawezi kusubiri kushurutishwa au ionekane kama vile anatoa hongo . Kipengele hiki kinawahusu wanaume zaidi .
2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .Hata kama ukiwa huna furaha , hujiona mwenye jukumu kuhakikisha unakuwa nayo kwa namna yoyote ile .
3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatajali umezungumza baya au zuri . Kwa bahati nzuri ni kwamba , ikiwa umekosea , yeye atachukua jukumu la kukuweka sawa.
Asiye na penzi la dhati, ukikosea kwake ni kichekesho . Badala ya kukurekebisha na kukuweka kwenye mstari, atakucheka .
4. Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha . Hatakuwa mtu wa kuviziavizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha . Kwake, shida yako itakuwa yake akiwa na imani kuwa , hata yake ni yako pia. Anayejiweka kando ukiwa na matatizo , siyo sahihi, mwepuke .
5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatapenda kuwa kikwazo cha maisha yako , atakulinda daima.Heshima ni msingi mkuu.
6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani . Pesa si kipaumbele chake.
7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine , hafichi hisia zake mbele za watu , atakutetea na kukufanya wa kwanza .
8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.
9. Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini , asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya
maamuzi magumu. Kikubwa ni kusimamia katika ukweli na masilahi yanayoeleweka .
10. Atakuwa tayari kuvumilia , hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe . Nimwelekezaji zaidi , hawezi kukurushia maneno ya kuudhi maana anajua kukuudhi aukukuumiza ni kuharibu maana nzima ya penzi lenu
MC.RAY
WhatsAPP 0659/375263
Face booke Raymond Mushi
Page Rashughuli
Histagram MC.RAYMONDMUSHI.
  
Kijana aliyetendwa na mpenzi wake aliyempenda sana.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni