Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumanne, 11 Novemba 2014

SIERRA L.KUWAFIDIA WALIOKUFA KWA EBOLA



 
 Wafanyakazi wa afya huko Sierra Leone
Serikali ya Sierra Leone imesema italipa dola elfu tano za kimarekani kama fidia kwa familia ya kila mfanyakazi wa afya ambaye amefariki baada ya kuambukizwa Ebola wakati akihudumia wagonjwa wa Ebola.
Kituo cha taifa cha kupambana na Ebola nchini humo kimesema fidia hiyo ya mara moja pia kwa ndugu wa wafanyakazi wa afya zaidi mia moja ambao wamekufa kwa ugonjwa huo hapo awali.
Virusi vya ugonjwa huo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini Sierra Leone ambapo katika muda wa siku tatu zilizopita zaidi ya watu mia tatu wamegundulika kuambukizwa ugonjwa huo.
Mwezi uliopita serikali ya Guinea nayo ilisema ingeanza kulipa dola elfu kumi kwa kila familia ya mfanyakazi wa afya aliyeambukizwa Ebola wakati akitekeleza majukumu yake.
chanzo.BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni