Polisi wa Ki Israel huko West Bank
Mwanamke mmoja mwenye asili ya
Israel ameshambuliwa kwa kisu na kusababisha kifo chake katika eneo la
West Bank, tukio hilo limepisha kwa saa moja baada ya askari mwenye
asili ya Israel pia kushambuliwa na kuumizwa vibaya mjini Tel Aviv.
Polisi wametoa taarifa ya kwamba washambuliaji wote wa majeruhi hao ni raia wa Palestina.Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kutumia kila mbinu ili kukomesha kabisa mashambulizi hayo.
Inasadikika kwamba mashambulio ya namna hii yametiwa kasi na suala la kuendelea kuwepo na mpango wa makazi mashamriki mwa Jerusalem na suala la haki ya kuabudu katika eneo nyeti la msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Jerusalem ambao pia hujulikana kama hekalu la milimani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni