Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 10 Novemba 2014

PACHA WANAOSHEA MWANAUME MMOJA




Pacha wanaofanana kwa kila kitu
Pacha waliozaliwa kwa kupishana dakika moja, wanashirikiana kila kitu maishani. Maisha ya kawaida, gari, akaunti ya facebook, benki, mshahara, kazi hata rafiki wa kiume, yote hayo wanafanya kwa kushirikiana.
Mabinti hao raia wa Australia, Anna na Lucy DeCinque (28), pia wanatumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya upasuaji wa kuondoa kitu chochote kitakachowafanya wasifanane.
Wamefanya upasuaji wa kuongeza matiti katika kiwango kimoja ufanano wao ubaki kama ulivyo, wametengeneza midomo, kope za kwenye macho na mambo mengine mengi ya kulinda namna wanavyotaka kufanana.
Matumizi yao ya kukarabati mwili yamewagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 217,430 (Sh365.6 milioni).
Ni nadra sana pacha hawa kutembea kila mtu kwa wakati wake, muda wote wanakuwa pamoja, wanalala muda mmoja, wanatumia gari moja na kitanda kimoja pia.
Pacha hawa wanaoishi katika mji wa Perth, Mashariki nchi ya Australia, bado wanaishi na mama yao anayeshuhudia namna mabinti zake wanavyopatana.
Ingawa kila mmoja ana utashi na vitu anavyopenda maishani, lakini wamechagua kuwa na rafiki wa kiume mmoja anayetoka nao wote kwa pamoja na wakati mmoja.
Anna na Lucy, wanaamini kuwa na rafiki mmoja wa kiume kunasaidia kujenga uhusiano wenye furaha tofauti kama kila mmoja angekuwa na mtu wake kama ilivyo kwa pacha wengi.
Rafiki yao wa sasa wa kiume, Ben Byrne ni fundi umeme anayeishi katika mji wa Perth.
Anna anasema: “Tuna mwanaume mmoja kwa ajili yetu. Katika uhusiano wetu, kuna watu watatu walioamua kufanya jambo moja bila ubaguzi, chuki wala kinyongo.”
Lucy anaongeza: “Ni kama inafurahisha kwetu. Tuna rafiki mmoja wa kiume tunalala naye kitanda kimoja. Kuna vijana wangependa kuwa na marafiki wawili wa kike kama ilivyo kwa Byrne.”
“Tuna ladha na hamu zinazofanana kwa kila kitu, hivyo siyo shida kumpenda mtu mmoja. Tuko pamoja kwa kila kitu, tunashirikiana kwenye mapenzi pamoja, tuko chumbani pamoja kufurahi na raf

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni