Rais Barack Obama na Angela Markel
Rais wa Marekani Barack Obama
amesema kuwa Marekani inatafakari kupeleka silaha nchini Ukraine
kusaidia kukabiliana na Waasi wanaoiunga mkono Urusi.
Akizungumza
katika Ikulu ya White House baada ya mazungumzo na Kansela wa Ujerumani
Angela Markel, Obama amesema nia itakuwa kuisaidia Ukraine kuimarisha
ulinzi kuliko kulishinda jeshi la Urusi. Lakini amesema ana matumaini
kuwa suluhu ya kidiplomasia itapatikana.“Ubabe wa Urusi umeimarisha umoja wa Marekani na Ujerumani na washirika wetu duniani kote na ningependa kumshukuru Angela kwa uongozi wake imara na ushirika wetu tunapokutana na changamoto hii.Tunaendelea kusisitiza kupatikana kwa suluhu kwa njia ya diplomasia”amesema Obama
Naye Kansela wa Ujerumani Angela Markel haoni kama njia za kijeshi zinaweza kuumaliza mzozo huu.
chanzobbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni