Tume ya uchaguzi ya Nigeria
imekutana na waakilishi wa vyama vyote vya siasa vilivyoandikishwa
kujadili iwapo uchaguzi mkuu wa Jumamosi (14/02/15) unafaa kuakhirishwa.
Rais
Goodluck Jonathan, magavana wa majimbo, wakuu wa jeshi, na ma-rais wa
zamani, wameiomba tume ya uchaguzi ijadili na pande zote kuhusu hali ya
usalama nchini.Kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, linafanya mashambulio makali kaskazini-mashariki mwa Nigeria ambako linadhibiti eneo kubwa.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni