Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema
Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro
Obiang Nguema , amesema yeye mwenyewe atalipa jumla ya tiketi elfu
arobaini kwa ajili ya wapenzi wa soka nchini mwake ili waweze kuhudhuria
mechi ya Kombe la Mataifa Afrika.
Michuano hiyo inayoanza
jumamosi, yalitangazwa kufanyika nchini humo baada ya kuthibitishwa kuwa
hayatafanyika morocco kama ilivyopaswa.Rais Obiang anasema anaona ni wajibu kwake na wengine wenye uwezo kununua tiketi kufanya hivyo akitoa wito wa kujaza viwanja. Ametoa wito kwa wale wenye uwezo wa kuwasaidia masikini kufanya hivyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni