Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumapili, 1 Februari 2015

KODI YA KUGHARIMU AU YAANZISHWA



Viongozi wa umoja wa mataifa nchini Adis Ababa Ethiopia 
Katika mkutano wa siku mbili wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, viongozi hao wamependekeza kuanzisha kodi ili kugharimia shirika hilo.
Wamependekeza kodi itozwe juu ya tikiti za ndege, hoteli, na ujumbe wa simu za mkononi.
AU zamani ikifadhiliwa na kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, lakini sasa bajeti yake inagharimiwa na wafadhili wa kimataifa.
Viongozi hao walipokutana mjini Addis Ababa, pia walisema kuwa mahakama ya Jinai ya kimataifa, ICC, inafaa kufuta mashtaka dhidi ya rais wa Sudan, Omar al-Bashir, na makamo wa rais wa Kenya, William Ruto.
AU imekuwa ikiilaumu ICC, kuwa mara nyingi inawalenga viongozi wa Afrik
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni