Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa.
Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka.
Mzozo wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya Watu na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.
Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini yalishindwa, kwa kuwa pande zinazokinzana zilishindwa kuunda Serikali ya umoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni