Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 5 Novemba 2014

PROGRAMU YA MASHOGA YAFADHILIWA UCHINA

 

Programu ya kuwaunganisha mashoga nchini Uchina imejipatia ufadhili wa dola millioni 30 kutoka kwa wawekezaji wa kampuni ya DCM.
Blued, iliobuniwa na mtandao wa jamii wa Danlan mwaka 2012 hutumiwa na takriban watu millioni 15.
Kulingana na mtandao wa habari wa Tech barani Asia,watumiaji hao wanaonekana kutoka katika miji mikuu mikubwa kama vile,Beijing,Shangai na Guangzou.
Ushoga nchini Uchina ulikuwa haramu hadi mwaka 1997 na ulionekana kama ugonjwa wa akili hadi mwaka 2001
Xiaofeng Wang ,ambaye ni mchambuzi katika kampuni ya utafiti ya Forrester ,amesema katika ripoti ya kampuni hiyo ya huduma za data kwamba programu za mesenja zina umaarufu mkubwa nchini Uchina kwa kuwa kasi ya mtandao wa simu iko chini.
Lakini katika kuchumbiana, programu hiyo hutumika wazi na wapenzi wa jinsia tofauti,programu moja ya kuchumbiana kwa jina Momo ina takriban watumiaji millioni 52.
Lakini upande wa mashoga swala hilo hufanywa kwa siri kubwa sana.''Huwezi kuwaona mashoga walio na ari ya kutangaza jinsia zao''.alisema Forrester.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni