
Askari polisi mwenye namba G.7168 PC Joseph Swai (29) ameuawa kikatili juzi asubuhi baada ya kukatwa na panga kichwani wakati akimuokoa mtoto mwenye umri wa miezi nane asiuawe na baba yake mzazi. Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, David Misime amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 5 asubuhi katika kata ya Chang’ombe Juu iliyopo katika Manispaa ya Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni