Salva Kirr
Rais wa Sudan Kusini , Salva Kiir,
na kiongozi wa waasi, Riek Machar, wametiliana saini kuundwa kwa
serikali ya kugawana madaraka kuhitimisha vita vya zaidi ya mwaka mmoja.
Makubaliano
hayo yamefikiwa katika mji mkuu wa Adiss Ababa, Addis Ababa.wanaume hao
wawili wamekubaliana kuhitimisha mapigano na vita vya wenyewe kwa
wenyewe mpaka kufikia March tano.Kwa muda kidogo washauri namna gani ya kuunda mfumo wa serikali ya kugawana madaraka.
Taarifa ambazo BBC haijazithibitisha zinaeleza kwamba Rais Salva Kiir atasalia kuwa Rais wa nchi hiyo na Riek Machar atateuliwa kushika wadhifa wa maakamu wa Rais. Vyama hivyo viwili viliingia kwenye mapigano mara tu baada ya Machar kutimuliwa kwenye wadhifa wa makamu raisi mnamo mwezi December mwaka 2013.
Mazungumzo kadhaa kama hayo ya kutafuta suluhu yalishindwa kuzaa matunda.
CHANZOBBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni