Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 5 Machi 2015

B FASSO;MWILI WA SANKARA KUFUKULIWA.

Mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina fasso marehemu Blaise Campaore kufukuliwa 
Serikali Burkina Fasso imeagiza kufukuliwa kwa mwili wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Thomas Sankara .
Watu wa familia ya rais huyo wamekuwa na wasiwasi kuhusu utambuzi wa maiti ya kiongozi huyo wa zamani.
Mjane wa marehemu Miriam,akizungumza kupitia njia ya simu kutoka Paris amesema, kuwa ufukuaji wa mwili huo utafanywa kulingana na agizo la mahakama ili kusaidia katika kuwatafuta waliotekeleza mauaji yake.
Bwana Sankara aliuawa mnamo mwaka wa 1987 katika mapinduzi yaliomfanya aliyekuwa rafikiye na mshirika wake mkuu Blaise Campaore kuchukua mamlaka.
Blaise Campaore aling'atuliwa mamlakani katika mapinduzi ya raia mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita.
Serikali mpya inayoongozwa na Michael Kafando ,imesema kuwa italiangizia swala hilo wakati ilipochukua hatamu.
Mwili wa Sankara ulizikwa katika kaburi lisilotambulika katika makaburi yaliopo mashiriki mwa mji wa Ouagadougou.
chanzo bbc

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni