Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumapili, 1 Machi 2015

NETANYAHU AWASILI MAREKANI .

 
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu 
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amewasili nchini Marekani kupinga dhidi uwezekano wa kufikia makubalino na Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.
Bwana Netanyahu anasema mkataba huo hautoshi kuizuia Iran kumiliki silaha za nyuklia.
Anatarajiwa kulihutubia Bunge la Congress Jumanne, hotuba ambayo haikukubaliwa kabla na utawala wa Rais Obama na kuiudhi Ikulu ya Marekani.
Hotuba hiyo inakuja wiki mbili kabla ya uchaguzi wa Israel, huku chama chake cha Likud kikiwa katika shinikizo katika uchaguzi wa nyumbani.
Marekani na mataifa mengine yanayotambulika kama P5+1 - wanajadiliana na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Wanataka mpango wa makubaliano kufikia mwishoni mwa mwezi huu ambao unaeleza wasiwasi kuwa Iran inatafuta teknolojia ya silaha za nyuklia, jambo ambalo linakanushwa na Iran.
Rais Obama hana mpango wa kukutana na Bwana Netanyahu
Wafuasi kadhaa wa Democrat akiwemo Makamu wa Rais Joe Biden amesema hatahudhuria hotuba hiyo.
chanzo bbc.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni