Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumapili, 1 Machi 2015

WASICHANA WALIOELEKEA SYRIA WAONEKANA.

 
 Wasichana wa Uingereza waliotorokea Syria kujiunga na IS waonekana katika kand ya Video
Kanda ya Video ya CCTV imeonyesha picha za wasichana watatu wa Uingereza waliotoroka makwao kuelekea nchini Syria ili kujiunga na wapiganaji wa IS.
Shamima Begum,Amira Abase wenye umri wa miaka 15 na kadiza Sultana mwenye umri wa miaka 16 walisafiri kutoka London kuelekea Istanbul tarahe 17 mwezi Februari.
Picha hizo zimewaonyesha wakisubiri katika kituo cha basi cha Bayrampasa baadaye siku hiyo.
Wapepelezi wa Scotland Yard wanaamini wanafunzi hao wa shule ya Bethnal Green Academy wameingia nchini Syria.
 
wasichana walioelekea Syria
Wanadaiwa kupokewa mpakani na wapiganaji wa Islamic State.
BBC inaelewa kwamba wasichana hao walingojea katika vituo wiwili vya mabasi kabla ya kuchukua basi la kuelekea Urfa karibu na mpaka wa Syria tarehe 18 Februari.
Kutoka kituo hicho wanadaiwa kupelekwa karibu na kivuko cha mpaka huo na wapiganaji hao.
Wakati katika kanda hiyo ya video unaonyesha kuwa wasichana hao walikaa katika kituo hicho kwa takriban saa 18.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni